Jumatano, 18 Aprili 2018

ZITAMBUE AINA ZA MARAFIKI ULIONAO


Marafiki ni watu muhimu sana katika maisha kwakua ndio huwa watu wetu wa karibu ambao huwa ni watu wa kwanza kujua hisia zetu katika mambo tofauti tofauti yanayo tusibu ikiwa ni pamoja na huzuni furaha zetu.

Rafiki ndio huwa taswira ya wewe ni nani na nini unapenda.
Miongoni mwa wahamasishaji maarufu ulimwenguni Dag Heward Mills alisema" show me who your friends are and i will tell you who you are", akiwa na maana nioneshe rafiki yako ni nani na nitakuambia wewe ni nani,hii ikimaanisha kupitia rafiki zako tunaweza jua unapenda nini,,nini hupendi, interest,hobby n.k.
Rafiki anaweza akachangia kupanua maono na mitazamo yako juu ya maisha au akaharibu.

Kwa mujibu wa mwanafalsafa maarufu Aristotle,kajaribu kuelezea aina kuu tatu za marafiki ambao kila mtu anakuwa nao katika maisha yake ya kila siku.

1.UTILITY FRIENDSHIP:, Hawa ni wale ambao urafiki wenu umejengwa katika mahusiano yenu ya kusaidiana katika mambo fulanifulani. Inawezekana mnasaidiana masomo,kazi,fedha n.k.
Sifa kubwa hapa ni kuwa urafiki unadumu kwasababu kila mmoja kuna wakati huwa anamsaidia mwenzake.

2.PLEASURE FRIENDSHIP; Urafiki huu umejengwa katika kuwa na mambo ya kiburudani ambayo mnayafurahia kwa pamoja. Mara nyingi hata kama hakuna kitu cha maana mnachokifanya pamoja lakini starehe,hobby au interest huwa zinawaunganisha pamoja. Inawezekana mnapenda kuangalia mpira wote, mnakutana bar kufurahia kinywaji n.k.
Watu wengi hufelishwa na marafiki wa namna hii kwa sababu wanawapa nafasi kubwa sana kwenye maisha yao wakati mwingine zaidi ya wenzi wao.

3.FRIENDSHIP FOR GOOD; Hawa ni marafiki ambao mnaunganishwa na malengo yanayofanana na mnathamini vitu vinavyofanana( goals and value). Urafiki huu huchukua muda mrefu sana kuujenga lakini ukipata mtu sahihi anaweza kuwa msaada mkubwa sana kwenye kukusaidia kutimiza ndoto zako.
Hawa hata kama hampati nafasi ya kuburudika pamoja ila mnakuwa na malengo mengi pamoja. Wengine hata msipowasiliana kwa muda mrefu mkikutana hakuna anayemlaumu mwenzake,mnakuwa kama mlikuwa wote siku zeto.

Je una behave vipi unapokutana na marafiki zako kwa kuzingatia sifa na kundi analokuwepo?

Ahsante sana ndugu msomaji kwa kusoma makala hii,kuna makala nyingine zaidi.


Na:Mussa kudonto

Adress:mkudonto@gmail.com
Contacts: 0657410894.

Maoni 1 :

  1. I have you as utility friend and Friendship for good,,hakika nimekuelewa sana.

    JibuFuta

ZITAMBUE AINA ZA MARAFIKI ULIONAO

Marafiki ni watu muhimu sana katika maisha kwakua ndio huwa watu wetu wa karibu ambao huwa ni watu wa kwanza kujua hisia zetu katika mamb...