MASOMO MANNE YENYE KULETA HAMASA KATIKA MAISHA YAKO.
Ni ukweli usiopingika kuwa karne ya Ishirini na moja(21) ni karne iliyoambatana na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia hali inayopelekea kuchangamana kwa jamii moja na nyingine katika nyaja mbalimbali za maisha ikiwemo kiuchumi,siasa na kijamii.
Hali hii ya uchangamano husababisha kubadilika kwa kifikra,mitazamo na misimamo miongoni mwa jamii zetu.
Katika pilikapilika za kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha watu wa lika tofauti tofauti wamekuwa wakijishughulisha katika shughuli mbalimbali za kiuchumi kwaajili ya kujitafutia ridhiki.
Neno mafanikio ni neno ambalo bila shaka limekuwa likitamkwa na takribani na watu wa umri tofauti tofauti hata mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitano anaweza kulitumia kuonesha matamanio(ambitions) zake pindi atakapokuwa mkubwa. Tatizo huja ni kwa namna gani tunaweza fikia adhima ya kuwa na mafanikio katika maisha yetu hususani pale unapoona mwingine kafanikiwa kwa kutumia njia fulani na pengine ukawaza labda utumie njia ileile ambayo jirani,rafiki ama watu mbalimbali wanaokuzunguka wamezitumia hadi kufanikisha malengo yao.
Maisha ya mwanadamu yameundwa kwa Mfano ambao kalamu(pencil) imeundwa,hivyo kupitia kalamu tunaweza pata taswira halisi ya maisha ya kila siku ya mwanadamu ambayo tuweza jifunza kupitia kalamu na kukapata mafunzo mbalimbali kama ifuatavyo;
1.KITU CHOCHOTE KIZURI KWAKO HUTEGEMEA ZAIDI MUITIKIO WAKO.
Kalamu imeundwa katika pande kuu mbili,ambazo ni upande wa nje ambao kwa muonekano huvutia kwa rangi na marembo mbalimbali yanayochangia kupendezesha na kuifanya ivutie kwa kila anayeitiziama. Na sehemu ya ndani ambayo imeundwa kwa risasi iliyojazwa ndani yake ambayo ndio msingi mkuu wa uwepo wake. Mgawanyiko huu wa kalamu huenda sambamba na vile mwanadamu anaishi,kwa kuwa pia tuna nje yetu ambayo hujumuisha muonekano wetu ambao unakuwa rahisi kuelezwa na yeyote yule atayeweza kukutazama.
2.KILICHOMO NDANI YAKO NDICHO KINACHOWEZA KULETA MATOKEO.
Kama ilivyo kalamu huwezi ona matakokeo yake ikiwa imekaa,hadi pale itakapo andikwa kwenye karatasi ndipo tutaona matokeo yake,vivyo hivyo mwadamu alivyo,,pindi atakapo toa yaliyo mjaza ndani ya moyo wake,fikara zake na mitazamo yake ndipo matokeo ya uwepo wake yatakapo anza kuonekana katika maisha yetu wakati mwingine hata wale wanaotuzunguka. Hii huenda sambamba na asili ya neno elimu ambayo ilichukua tafsiri yake kutoka lugha kilatini(educare) ambayo kwa lugha ya kiingereza ni (education--brings out),ikiwa na maana ya kutoa nje kwa tafsiri ya moja kwa moja katika lugha ya kiswahili. Hapa tunajifunza kwamba njia pekee ya kufanya uwe na matokeo juu ya wewe ni nani, ni kutoa ulichonacho kwakuwa ndio kitu pekee kitakacho tengeneza charisma yako. Unaweza kuwa na muonekano unaovutia machoni mwa watu lakini ukiwa mkweli,mwema na mwenye upendo huleta hamasa. Pia ni kweli kwamba haiba zetu zinaweza vutia lakini tabia zetu na matendo yetu huleta hamasa juu yako. Mfano mzuri ni hadithi ya Thomas Alva Edison,mgunduzi mkubwa wa karne aliyegundua bulb(tuberight) ambazo zimekuwa chanzo kikubwa cha mwanga ulimwenguni karne ya ishirini na moja.
Thomas Edison alipewa barua na mwalimu wake aipeleke nyumbani hivyo ni mamaake pekee ndio alitakiwa aifungue barua ile. Thomas kwa utiifu uliotukuka akafanya kama alivyoagizwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani Thomas alimkabidhi ile barua mamaake. Mamaake Thomas kaifungua ile barua na kuanza kuisoma, baada ya dakika Mamaake Thomas akaanza kububujikwa na machozi. Thomas alikosa ujasili wa kuvumilia hivyo ilimbidi amuulize mamaake kulikoni mbona analia. Mamake Thomas kajibu "Thomas mwalimu wako kaandika kuwa,Thomas ni kijana mwenye akili sana, pia ni genius. Hivyo kwa udogo wa shule yetu haina walimu wazuri wa kutosha kwaajili ya kumfundisha ,ni bora asije shule tena na wewe mamaake ndio umfundishe akiwa nyumbani.
Miaka kadhaa baadae wakati mamaake Thomas akiwa amesha fariki na Thomas akiwa tayari ni miongoni mwa wagunduzi wa karne,Thomas alikuwa katika nyumba ya mamaake akifanya usafi,,wakati anaendelea kufanya usafi kavuta droo ndogo ya kabati na kukuta vipande vidogo vya karatasi vimefungwa pamoja.Baada ya kuangalia kwa makini aligundua kuwa ni barua aliyopewa na mwalimu wake miaka kadhaa iliyopita. Thomas Alva Edison alifungua ile barua na kuanza kuisoma,baada ya dakika alianza kulia kwa uchungu sana kwakuwa kilichoandikwa kwenye ile barua ni kuwa;.
" Madam,mwanao Thomas ni mbumbumbu,ana matatizo ya akili,hatufai hapa shuleni kwetu, na sidhani kama anaweza kusoma shule yeyote,hivyo kuanzia leo tumemuonda hapa shuleni".
Thomas baada ya kuimaliza kuisoma akaandika chini ya ile barua "Thomas kweli ni mbumbumbu ana matatizo ya akili na amefanikiwa kufanya ugunduzi mkubwa chini ya uangalizi na usimamizi wa shujaa wake pekee ambaye ni mamaake".
Hadithi hii ya Thomas edisom hutuonesha ni kwa namna gani mamaake na Thomas kuwa hakuwa na muonekano uliomfanya awe maarufu,hakuwa na haiba iliyomfanya awe maarufu lakini alikuwa na upendo na tabia ambayo ilikuwa na matokeo chanya kwa Thomas.
3.HUWEZI PATA BILA KUPITIA MAUMIVU NA CHANGAMOTO.
Moja kati ya maelekezo muhimu watengenezaji wa kalamu wameyaweka bayana ni yale yanayoelezea ni kwa namna gani unaweza ifanya kalamu yako ikawa inaendelea kuandika kwa maandishi mazuri yenye kuonekana ni kupitia kuchongoa kalamu yako kwa chongeo lenye makali ili upate incha sahihi kulingana na matumizi yako. Mwanadamu ameumbwa na ubongo unaofanya kazi ya kuratibu matendo mbalimbali katika maisha yake ya kila siku. Katika mwili wa binadamu kuna viungo mbalimbali vyenye kufanya kazi tofauti tofauti. Kama ilivyokwa binadamu ili aweze kuendelea kuishi ni lazima awe anapata chakula kwaajili ya nguvu na ukuaji, ubongo wa mwanadamu pia unahitaji mawazo yenye kumjenga kwa kuulisha fikra na positive attitudes zinazoweza kubadili mitazamo yake na kuwa positive thinker.
Kitu chamsingi ni kwamba wakati tunafanya juhudi kufikia malengo kuna changamoto mbalimbali unaweza kabiliana nazo hivyo kikubwa ni kuwa na msimamo na malengo juu ya nini na kwa wakati gani unataka ukipate.
4.TAMBUA MAKOSA YAKO, YAREKEBISHE NA UANZE UPYA.
Ukiwa katika safari yako ya maisha unaweza kumbana na mitihani midogomidogo ambayo inaweza changia kwa namna moja ama nyingine kukufanya ukate tamaa na kujikuta huna ujasiri,nguvu wala hamasa ya kuendelea na kile kitu. Waliotengeneza kalamu waligundua na kutambua kuwa kuna wakati mtu hawezi kuwa sawa asilimia zote hivyo kujikuta hukosea wakati ukiandika ndipo waliona nivema kukawa na futio(eraser),ambao unampa fursa mwandishi kufuta pale alipokosea na kuanza upya.
Unapokumbana na hali kamai hii katika maisha yako angalia umekose wapi,ukishagundua fanya marekebisho then anza upya ukiweka akilini juu ya pale ulipokosea.
Finally according to my favorite mentor shiv khela said" we need to compete for knowledge and wisdom,not for grades . Knowledge is pilling up facts, wisdom is simplifying learning much. The most important thing one can learn is to "learn to learn".
People confuse education with the ability to memorize facts. Education of the mind without morals creates menace to society.
Ahsante kwa kusoma makala hii,kuna makala nyingine zaidi kwaajili yako.
Na: Mussa Kudonto
Adress: mkudonto@gmail.com
Contacts:0657410894
Blogu hii ni maalumu kwajili ya masomo mbalimbali yanayohusu maisha,ujasilia mali na ushauri juu ya nyanja mbalimbali za maisha
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
ZITAMBUE AINA ZA MARAFIKI ULIONAO
Marafiki ni watu muhimu sana katika maisha kwakua ndio huwa watu wetu wa karibu ambao huwa ni watu wa kwanza kujua hisia zetu katika mamb...
-
Marafiki ni watu muhimu sana katika maisha kwakua ndio huwa watu wetu wa karibu ambao huwa ni watu wa kwanza kujua hisia zetu katika mamb...
-
MASOMO MANNE YENYE KULETA HAMASA KATIKA MAISHA YAKO. Ni ukweli usiopingika kuwa karne ya Ishirini na moja(21) ni karne iliyoambatana n...
Congrats brother,nashukuru kwa somo lako zuri,kuna kitu nimejifunza.
JibuFuta